Kanuni ya Maadili ya Murad kwa Kiswahili
Kufuatia maoni na mapendekezo muhimu na ya kina yaliyotolewa wakati wa mashauriano ya kiulimwengu kuhusu Rasimu ya Kanuni ya Maadili ya Murad, mchakato wa kina wa mapitio na marekebisho umekamilika. Mchakato huu wa marekebisho ulihusisha waathiriwa na wataalamu wengine kupitia mapitio ya maandishi na warsha kuhusu marekebisho ya rasimu. Mchakato huu umezalisha toleo la ‘kutumika’ la Kanuni ya Maadili ya Murad (“Kanuni ya Maadili ya Kimataifa ya Kukusanya na Kutumia Taarifa Kuhusu Ukatili wa Kingono wa Kimfumo na Unaohusiana na Migogoro”), iliyotolewa tarehe 13 Aprili 2022.
Toleo la Kiswahili la Kanuni ya Maadili ya Murad lipo hapa chini. Kanuni hii ya maadili ni hati hai ambayo itapitiwa mara kwa mara ili kuhakikisha inaendelea kuonyesha viwango ambavyo haviwezi kupunguzwa vya ukusanyaji salama, wenye ufanisi na wa kimaadili wa maelezo kuhusu ukatili wa kingono wa kimfumo na unaohusiana na migogoro (SCRSV).